Saturday, August 6, 2016

PIGO: ARSENAL KUANZA LIGI NA LIVERPOOL BILA MESUT OZIL, OLIVIER GIROUD AND LAURENT KOSCIELNY

Mesut Ozil, Olivier Giroud na Laurent Koscielny wataikosa Mechi ya kwanza kabisa ya Msimu Mpya wa Ligi Kuu England ya Arsenal dhidi ya Liverpool ya Jumapili Agosti 14.

Watatu hao bado hawajarejea Mazoezini baada ya kupewa nyongeza ya Vakesheni kutokana na ushiriki wao kwa Nchi zao Germany na France zilizocheza EURO 2016 iliyomalizika Julai 10.
Pengo hilo linamuacha Arsene Wenger akiwa na uhaba mkubwa hasa baada ya Sentahafu Per Mertesacker kuumia Goti na sasa kupaswa kukaa nje kwa muda mrefu.
Mara baada ya Jana kuifunga Viking FK 8-0 huko Norway, Wenger alitoboa upungufu huo ambao sasa utamfanya awatumie Gabriel, Calum Chambers na Mchezaji mpya Rob Holding kama Mabeki wake.
LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17
RATIBA:
Jumamosi Agosti 13

14:30 Hull City v Leicester City
17:00 Burnley v Swansea City
17:00 Crystal Palace v West Bromwich Albion
17:00 Everton v Tottenham Hotspur
17:00 Middlesbrough v Stoke City
17:00 Southampton v Watford
19:30 Manchester City v Sunderland

Jumapili Agosti 15

15:30 A.F.C. Bournemouth v Manchester United
18:00 Arsenal v Liverpool

Jumatatu Agosti 16

22:00 Chelsea v West Ham United