Sunday, August 7, 2016

POGBA HUYOO KWENYE VIPIMO TAYARI KUJIUNGA NA MAN UNITED

Paul Pogba ameruhusiwa na Klabu yake Mabingwa wa Italy Juventus kuruka kwenda Jijini Manchester kupimwa Afya yake ili kukamilisha Uhamisho kurudi tena Manchester United.
Taarifa hizi zimetolewa na Msemaji wa Juventus kutoka Turin, Italy.
Kiungo huyo wa France mwenye Miaka 23 na ambae aliihama Man United Miaka Minne iliyopita na kutua Juve bila Man United kuambulia Ada yeyote mbali ya Fidia ya Pauni Laki 8 kwa kukuza Kipaji chake sasa atarejea Old Trafford kwa Dau linalodaiwa ni Rekodi ya Dunia.
Hilo kuwa Rekodi ya Dunia kwa Uhamisho wa Mchezaji halijathibitishwa na Klabu zote mbili lakini tamko hilo la Juve ambalo pia limerushwa rasmi kwenye Tovuti ya Klabu ya Man United sasa linathibitisha Uhamisho huu.

Ikiwa Pogba atatua Man United atakuwa Mchezaji wa Nne baada ya Meneja Mpya kuwasaini Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic na Hendrik Mkhitaryan.