Friday, August 5, 2016

UEFA CHAMPIONS LIGI: MAN CITY USO KWA USO NA STEAU BUCHAREST ILI KUFUZU MAKUNDI

Manchester City itabidi iitoe Steaua Bucharest ya Romania ikiwa itataka kutinga Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

Mechi hiyo imepangwa katika Droo iliyofanyika huko Nyon, Uswisi hii Leo na Mechi za Raundi ya Mwisho za Mchujo zitachezwa Agosti 16 na 17 na Marudiano ni Agosti 23 na 24.

Washindi wa Raundi hii watatinga kwenye Makundi ambapo Droo yake itafanyika Agosti 25.
DROO KAMILI:
Ludogorets Razgrad vs FC Viktoria Plzen
Celtic vs Hapoel Beer-Sheva
FC Copenhagen vs Apoel Nicosia
Dundalk vs Legia Warsaw
Dinamo Zagreb vs FC Salzburg
Steaua Bucharest vs Manchester City
FC Porto v Roma
Ajax vs Rostov
Young Boys vs Borussia Monchengladbach
Villarreal vs Monaco

UCL 2016/17
-KUANZIA Hatua ya Makundi [Droo kufanyika Agosti 25]:
Chungu Na 1 (Mabingwa Watetezi na Timu 7 toka Nchi 7 za juu kwa Ubora Ulaya]
Real Madrid (ESP, Mabingwa)
Barcelona (ESP)
Leicester City (ENG)
Bayern München (GER)
Juventus (ITA)
Benfica (POR)
Paris Saint-Germain (FRA)
CSKA Moskva (RUS)

VYUNGU VINGINE:
Atlético Madrid (ESP)
Borussia Dortmund (GER)
Arsenal (ENG)
Sevilla (ESP)
Napoli (ITA)
Bayer Leverkusen (GER)
Basel (SUI)
Tottenham Hotspur (ENG)
Dynamo Kyiv (UKR)
Lyon (FRA)
PSV Eindhoven (NED)
Sporting CP (POR)
Club Brugge (BEL)
Beşiktaş (TUR)