Tuesday, August 9, 2016

UEFA SUPER CUP: REAL MADRID 3 v 2 SEVILLA FC

USIKU HUU huko Lerkendal Stadion, Trondheim, Nchini Norway kwenye Mechi ya kufungua dimba Msimu mpya wa 2016/17 wa UEFA wa Mashindano yao ya Klabu huko Ulaya ilichezwa Mechi kati ya Mabingwa wa Msimu uliopita, Mabingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI, Real Madrid, na Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI, Sevilla, zote za Spain, na Real kuibuka kidedea kwa Bao 3-2 katika Dakika 120 za Mchezo baada ya Sare ya 2-2 katika Dakika 90.

Real Madrid, Mabingwa wa Ulaya, wakicheza bila ya Mastaa wao wakubwa Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Toni Kroos na Pepe,walitangulia kufunga Bao Dakika ya 21 kwa Bao la Chipukizi Marco Asensio Willemsen aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza kabisa.
Sevilla walisawazisha Dakika ya 41 kwa Bao la Franco Vazquez.
Bao hizo zilidumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili Dakika ya 71 Yevhen Konoplyanka aliifungia Bao la Pili kwa Penati ya utata iliyotolewa na Refa wa Serbia Milorad Mažić aliedai Kepteni wa Real Sergio Ramos alimwangusha Vitolo.
Huku Dakika zikiyoyoma na Bango la Dakika za Majeruhi likiashiria zipo Daki za Ziada 4, Kepteni Sergio Ramos aliisawazishia Real Dakika ya 93 kwa Kichwa baada ya kuunganisha Krosi safi ya Lukas Vazquez.
Mechi ikaingia Dakika za Nyongeza 30.
Dakika ya 2 tu ya Dakika za Nyongeza 30, Sevilla wakabaki Mtu 10 baada ya Beki wao Timothée Kolodziejczak ‘Kolo’ kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 98, Real walipata Bao la 3 kupitia Sergio Ramos lakini Refa Msaidizi akalikataa bila kadamnasi kujua nini kilitokea.

Hadi Dakika 105 zinamalizika Bao zilibaki 2-2 na Timu kwenda Mapumziko mafupi.
Kipindi cha Pili cha Dakika za Nyongeza 30, Real waliendelea kuwa juu wakitumia mwanya wao wa kuwa na Mtu Mmoja wa ziada.

Fulbeki wa Kulia Dani Carvajal Dakika ya 118 alifunga Goli safi la kibinafsi baada ya kumpokonya Mpira Konoplyanka Winga ya Kulia na kuwatambuka wachezaji kadhaa wa Sevilla na kufunga Bao la 3 na la ushindi.

VIKOSI VILIVYOANZA:
REAL MADRID:
Casilla; Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo; Casemiro, Vazquez, Kovacic; Morata, Isco, Asensio
Akiba: Yanez, Nacho, Benzema, James, Modric, Danilo, Llorente

SEVILLA: Rico; Pareja, Carrico, Kolo; Kiyotake, N'Zonzi, Iborra, Vazquez; Mariano, Vietto, Vitolo
Akiba: Soria, Kranevitter, Rami, Ben Yedder, Sarabia, Escudero, Konoplyanka
REFA: Milorad Mažić [Serbia]