Thursday, August 4, 2016

UHAMISHO 2016: GABRIEL JESUS ATUA MAN CITY

Manchester City wamemsaini Winga wa Miaka 19 kutoka Brazil Gabriel Jesus wa Klabu ya Palmeiras kwa Dau la Pauni Milioni 27 likiwa na nyongeza kadhaa juu yake.

Jesus, ambae amesaini Mkataba wa Miaka Mitano na City, atabakia na Palmeiras hadi Desemba ambapo Msimu wa Soka wa Brazil utakapokamilika.

Kijana huyu ndie amewika kuwa Chipukizi mwenye kipaji cha juu huko Brazil na sasa yupo na Timu ya Brazil itakayocheza Michezo ya Olimpiki huko Brazil inayoanza Alhamisi Agosti 4.

Akiwa na Palmeiras, Jesus amefunga Bao 26 kwa Mechi 67 na Msimu huu, kwenye Ligi Serie A ya Brazil, yeye ndio anaongoza kwa Ufungaji Bora.