Saturday, August 6, 2016

UHAMISHO 2016: LLORENTE ATUA SWANSEA, TAYARI KWA MSIMU MPYA 2016/17

Fernando Llorente, Straika wa zamani wa Athletic Bilbao na Juventus  ambae Mwezi Mei alitwaa UEFA EUROPA LIGI akiwa na Sevilla, amesainiwa na Swansea City kwa Dau ambalo halikutajwa.

Llorente, mwenye Miaka 31, amesaini Mkataba wa Miaka Miwili.
Leo Straika huyo anaweza akaichezea Swansea kwa mara ya kwanza wakiwa kwao Liberty Stadium kucheza Kirafiki na Stade Rennais.

Ujio wa Llorente utaipa Swansea nguvu mpya baada ya kuondokewa na Mastraika wao Alberto Paloschi, Bafetimbi Gomis na Eder alieifungia Portugal Bao la ushindi kwenye Fainali ya EURO 2016 Mwezi Julai walipoibwaga France 1-0.

Jumamosi ijayo Swansea itaanza Msimu wao mpya wa Ligi Kuu England kwa kucheza na Burnley.