Thursday, August 4, 2016

UHAMISHO 2016: MABINGWA LEICESTER WAMNASA STAA WA POLAND KAPUSTKA

MABINGWA wa England Leicester City wamemsaini Winga wa Poland Bartosz Kapustka kutoka Cracovia kwa Uhamisho ambao unasubiri Baraka za Uhamisho wa Kimataifa.
Kapustka, mwenye Miaka 19, amenunuliwa kwa Dau la Pauni Milioni 7.5 na kupewa Mkataba wa Miaka 5.
Kijana huyo aling’ara huko France kwenye EURO 2016 akiichezea Poland Mechi 4 kati ya 5.

Kapustka anakuwa Mchezaji wa 5 kusainiwa na Meneja wa Leicester Claudio Ranieri katika kipindi hiki na wengine ni Kipa Ron-Robert Zieler, Beki Luis Hernandez, Kiungo Nampalys Mendy na Fowadi Ahmed Musa.