Saturday, August 6, 2016

UHAMISHO 2016: PAPY DJILOBODJI ANG’OKA CHELSEA NA KUTUA SUNDERLAND

Sunderland imemsaini Papy Djilobodji kutoka Chelsea kwa Dau la Pauni Milioni 8 na kuwa Mchezaji wa kwanza kusainiwa na Meneja wao mpya David Moyes.
Papy Djilobodji, Mchezaji wa Kimataifa wa Senegal, alinunuliwa na Chelsea kutoka Nantes ya France lakini alicheza Mechi 1 tu lakini hivi karibuni aliichezea Chelsea chini ya Meneja mpya Antonio Conte walipocheza Kirafiki na Rapid Vienna.
Djilobodji, mwenye Miaka 27, Msimu uliopita alikuwa kwa Mkopo huko Germany akiichezea Werder Bremen

Sunderland wamekuwa na mafanikio mazuri kwenye Mechi zao za majaribio na Jana walitoka Sare 1-1 na Borussia Dortmund huko Austria.
Sunderland wataanza Msimu mpya wa Ligi Kuu England Wikiendi ijayo kwa kucheza na Manchester City ambao nao wako na Meneja mpya Pep Guardiola.