Sunday, August 7, 2016

UHAMISHO: ANDRE AYEW HUYOO WEST HAM

West Ham United imeafiki Ada ya Pauni Milioni 20 kumsaini Staa kutoka Ghana Andre Ayew kutoka Swansea City.
Ayew, mwenye Miaka 26 na ambae alisainiwa na Swansea Mwaka 2015 bure bila Ada kutoka Klabu ya France Marseille, ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Swansea Msimu uliopita akiwa na Bao 12.

Hivi sasa Ayew, ambae ni Mtoto wa Lejendari wa Ghana Abedi Pele, anakamilisha makubaliano ya maslahi yake binafsi na West Ham.

Kwa kipindi hiki, West Ham ishamsaini Straika Ashley Fletcher, Kiungo Havard Nordtveit, na Mawinga Sofiane Feghouli na Gokhan.
Lakini pia zipo habari kuwa Meneja wa West Ham, Slaven Bilic, anataka kumchukua mdogo wake Andre, Jordan Ayew, kutoka Aston Villa ajiunge na Timu yake pamoja na Kaka yake.