Sunday, August 7, 2016

UHAMISHO: CITY YAMCHUKUA MORENO

Manchester City wamemsaini Fowadi wa Colombia Marlos Moreno kwa Dau la Pauni Milion 4.75 kwa Mkataba wa Miaka Mitano kutoka Atletico Nacional.
Kijana huyo wa Miaka 19 hatakaa City kwa Msimu huu unaokuja wa 2016/17 na badala yake atapelekwa huko Spain kucheza kwa Mkopo kwenye Klabu ya Deportivo La Coruna.

Moreno anakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Meneja mpya wa City Pep Guardiola Wiki hii baada ya pia kuwasaini Winga Leroy Sane toka Schalke ya Germany na Fowadi Gabriel Jesus wa Palmeiras ya Brazil.
Lakini Jesus atabaki huko Palmeiras hadi Januari 2017 na kwenda Etihad baada ya Msimu wa Brazil kumalizika.