Tuesday, August 2, 2016

UHAMISHO: KLABU YA SOUTHAMPTON YASAJILI WACHEZAJI WAWILI KWA MPIGO!

Southampton imemsaini Kipa wa Crystal Palace Alex McCarthy kwa Dau ambalo halikutajwa na pia Beki wa Kulia kutoka France Jeremy Pied kwa Uhamisho wa Bure.

McCarthy, mwenye Miaka 26, alikaa Msimu mmoja tu huko Palace baada ya kuhamia kutoka QPR Msimu uliopita na amesaini Dili ya Miaka Mitatu na Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’.

Beki Pied, mwenye Miaka 27, aliwahi kuchezea chini ya Meneja mpya wa Southampton Claude Puel walipokuwa Nice Msimu uliopita.
Mfaransa huyo amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na anakuwa Mchezaji wa Nne kusainiwa na Southampton katika kipindi hiki.

Wapya wengine waliosainiwa na Southampton ni Nathan Redmond kutoka Norwich na Pierre-Emile Hojbjerg kutoka Bayern Munich.