Wednesday, August 31, 2016

UHAMISHO: MIDDLESBROUGH YAMSAINI KWA MKOPO CHAMBERS WA ARSENAL

Middlesbrough wamemsaini Beki wa Arsenal Calum Chambers kwa Mkopo wa Msimu mmoja.
Chambers, mwenye Miaka 21 na ambae ana uwezo wa kucheza kama Fulbeki wa Kulia au Sentahafu, alijiunga na Arsenal Mwaka 2014 kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 16.
Chambers anakuwa Mchezaji wa 11 kusainiwa na Meneja wa Boro Aitor Karanka wakiwemo Kipa Victor Valdes, Straika Alvaro Negredo na Kiungo Marten de Roon.
http://65.media.tumblr.com/f5e6518999fb2eadb03aa0d870c00048/tumblr_nedez9memN1tihaueo1_1280.jpg