Thursday, August 4, 2016

UHAMISHO: MOHAMED SALAH APATA MKATABA WA KUDUMU AS ROMA

WINGA wa Chelsea Mohamed Salah sasa yupo rasmi AS Roma kwa Mkataba wa kudumu.
Salah, Mchezaji wa Kimataifa wa Egypt mwenye Miaka 24, alikuwa kwa Mkopo huko Italy akiichezea AS Roma Mechi 34 Msimu uliopita.
Kabla ya Msimu huo, Salah alikuwa huko huko Italy akichezea Klabu nyingine ya Serie A Fiorentina kwa Mkopo.

Salah alisainiwa na Chelsea Januari 2014 kutoka FC Basel ya Uswisi kwa Dau la Pauni Milioni 11 kwa Mkataba wa Miaka 5 na Nusu na kuchezea Mechi 13 tu.