Thursday, August 11, 2016

UHAMISHO: VIJANA WAWILI PADDY MCNAIR NA DONALD LOVE HAOO WASAJILIWA NA SUNDERLAND KWA DAVID MOYES!

Sunderland yawasaini Mabeki Wawili wa Manchester United Paddy McNair na Donald Love kwa Dau la Jumla la Pauni Milioni 5.5.
Chipukizi hao wote wenye Miaka 21 wamesaini Mkataba wa Miaka Minne kila mmoja chini ya Meneja Mpya wa Sunderland, David Moyes, ambae alitimuliwa Man United Miaka Miwili iliyopita baada ya kudumu Miezi 10 tu.
McNair, ambae aliwakilisha Nchi yake Northern Ireland huko Euro 2016, aliichezea Timu ya Kwanza ya Man United kwa mara ya kwanza Septemba 2014 na kucheza Jumla ya Mechi 27. Love, ambae ni Raia wa Scotland, alikuwa kwa Mkopo huko Wigan Msimu uliopita na amewahi kuichezea Timu ya Kwanza ya Man United mara 2.