Thursday, August 11, 2016

UHAMISHO: WEST HAM WAMSAINI JONATHAN CALLERI

West Ham imemsaini Straika wa Argentina Jonathan Calleri kwa Mkopo wa Msimu Mmoja kutoka Klabu ya Uruguay' Deportivo Maldonado.
Calleri, mwenye Miaka 22, aliwakilisha Argentina huko Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki ambako Jumatano Usiku ilitupwa nje baada ya kushindwa kuvuka Kundi lao.

Calleri alikuwa huko Brazil kwa Mkopo kwenye Klabu ya Sao Paolo na kuwa Mfungaji Bora kwenye Copa Libertadores.

West Ham, chini ya Meneja Slaven Bilic, itafungua dimba Msimu wao mpya wa Ligi Kuu England Jumatatu Usiku kwa kucheza Ugenini huko Stamford Bridge na Chelsea.