Saturday, August 13, 2016

VIFAA VYA UMALIZIAJI WA UWANJA WA KAITABA BUKOBA VYAFIKA LEO HII SIKU MOJA KABLA YA MKUTANO MKUU WA KRFA.


Mafundi wakishusha Vifaa mbalimbali ndani ya Uwanja wa Kaitaba hii leo kwa ajili ya umaliziaji wa Uwanja wa Kaitaba. Vikiwemo Mchanga, Gundi, Magoli, uzio wa bembeni ya Uwanja n.k leo hii Jumamosi siku moja kabla ya Uchaguzi wa KRFA ambao unatarajiwa kufanyika kesho Misenyi Bukoba. Picha zote na Faustine Ruta/bukobasportsMoja ya Kifaa maalum kilicholetwa leo hii cha kusambazia Rubber kwenye Uwanja wa Kaitaba ambao unajengwa kisasa kwa kuwekewa nyasi bandia, ambao hivi karibuni utamalizika na hatimaye kutumika kwa michezo mbalimbali. Gundi maalum ambayo ndio ilisimamisha kiasi kikubwa cha kuendelea kumalizika kwa Uwanja wa Kaitaba ikiwa tayari imefika na sasa kazi hiyo itakwenda kwa kasi sana.
Ndinga iliyoleta Vifaa ikiwa imepaki kushusha vifaa hiyo kwenye lango kuu la Kaitaba
Wakiendelea kushusha vifaa
Viongozi wa Soka wakiteta jambo baada ya Vifaa vya umaliziaji kufika Uwanjani hapo leo hii wakiteta jambo. kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama akiwa  na Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF Peregrinus Rutayuga.
Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF Peregrinus Rutayuga akiteta jambo kwenye simu mara baada ya Vifaa hivyo kufika Kaitaba na kuvishuhudia.
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama akipata jambo kuhusu umaliziaji wa Uwanja sasa mara baada ya Vifaa kufika. Ambapo aliweza kuambiwa kwamba zoezi la umaliziaji sasa linaanza haraka na litachukua siku 7-14 kumalizika na Timu ya hapa Bukoba Kagera Sugar inayocheza Ligi kuu VPL itapata fursa ya kuutumia kama hapo awali na ukiwa umeboreshwa kwa hali ya Kisasa tofauti na hapo nyuma.
Wakiwa mbele ya baadhi ya Vifaa vilivyofika hii leo

Kwanza zipo ngapi? Fundi akihesabu idadi ya Ndoo zilizobeba Gundi
Taswira mbalimbali za Uwanja wa Kaitaba hii leo

Mafundi wakiendelea na zoezi la kusambaza rubber kwenye Uwanja.