Saturday, August 27, 2016

WENGER ANYAKUA WAWILI WA LA LIGA, MUSTAFI NA PEREZ

BEKI wa Germany Shkodran Mustafi na Straika wa Spain Lucas Perez Jana walitarajiwa kukamilisha upimwaji wao wa Afya zao ili kusaini Mkataba na Arsenal.
Arsenal walishaafikiana na Valencia ili kumnunua Mustafi, mwenye Miaka 24, kwa Dau la Pauni Milioni 35 na ushei huku pia wakikubaliana na Deportivo La Coruna kumchukua Perez, 27, ambae akifunga Bao 17 katika Gemu 37 Msimu uliopita.
Dau la Perez limetajwa kuwa ni Pauni Milioni 17.1.
Wachezaji hao wanaungana na Wapya Viungo Granit Xhaka na Kelechi Nwakali, na Fowadi Takuma Asano.

Kwa kuwachota Mustafi na Perez, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger sasa ameelekea kujibu mapigo ya kwamba yu mgumu kutoa Fedha kununua Wachezaji Wapya.
Akiongea hapo Jana, Wenger alisema Klabu yao ipo kwenye mazungumzo na ana Imani watafanikiwa kuzikamilisha Dili hizo kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa Agosti 31 Saa 7 Usiku, Saa za Bongo.
Wenger ameeleza: “Safari hii ni Dirisha la Uhamisho la ajabu. Nilidhani litakuwa rahisi lakini ni gumu kupita yote ya nyuma!”

Kati ya Wapya wao, Mchezaji wa Japan Asano Takuma, alienunuliwa kutoka Sanfrecce Hiroshima Mwezi Julai, atajiunga kwa mkopo huko Bundesliga kuichezea Stuttgart kwa Msimu Mmoja.