Tuesday, August 2, 2016

YANGA YAITISHA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA JUMAMOSI HII.

Klabu ya Yanga Leo imetoa Taarifa ya kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama bila ya kufafanua ni Ajenda yake.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo ambayo ilisainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Mabingwa hao wa Tanzania Bara, Baraka Deusdedit, Mkutano huo utafanyika Jumamosi Agosti 6 huko Bwalo la Maafisa wa Polisi, Oyster Bay Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo pia ilibainisha kuwa Siku hiyo hiyo, Yanga watacheza Mchezo wa Kirafiki na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Habari za hivi punde zilizozagaa zimedai Mkutano Mkuu utafanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall huko Upanga Jijini Dar es Salaam badala ya Bwalo la Maafisa wa Polisi Siku hiyo hiyo Jumamosi Agosti 6.