Friday, August 5, 2016

YANGA YAWEKA WAZI AJENDA ZAKE KUELEKEA MKUTANO WAKE MKUU WA DHARULA, KUIGUSA KATIBA.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUELEKEA Mkutano Mkuu wa wanachama wa Yanga ulioitishwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji , Uongozi wa Yanga kupitia kwa mratibu wa Matawi na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Omary Kaya amezitaja ajenda kuu zitakazotumika kwenye mkutano huo huku suala la Mabadiliko ya Katiba ya Yanga yakipewa kipaumbele. Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kesho siku ya Jumamosi unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama wanaotaka kufahamu mwenendi mzima wa timu ya yao.