Thursday, September 22, 2016

BALOTELLI ATINGISHA DABI YA RIVIERA, KOCHA WAKE APIGWA BUTWAA!

BOSI wa Nice Lucien Favre ameungama kwamba Mario Balotelli sasa amezidi matarajio yao baada ya Jana kupiga tena Bao 2 kwenye Mechi na Monaco ya Ligi 1 huko France.
Hiyo ni Mechi ya pili mfululizo kwa Balotelli kufunga Bao baadavya Jana Nice kuwachapa Monaco 4-0 katika Dabi ya Riviera na kukaa kileleni mwa Ligi 1 wakiwa juu ya Mabingwa Watetezi Paris Saint-Germain.
Baada ya Gemu hiyo Kocha Favre alisema: "2-0 toka kwa Balotelli zilikuwa ni muhimu na zilitupa morali ya kujiamini. Mario ni muhimu kwetu kwani anatoa kina kwenye Gemu yetu. Sasa anapaswa kuendelea hivi hivi."
Kocha huyo aliendelea: "Baada ya Miaka kadhaa migumu kwake sasa anaweza kurejea kileleni. Tutajaribu kumsaidia ili aimarike zaidi!"
Aliongeza: "Bao 4 Gemu 2? Sikutegemea hilo!"