Wednesday, September 14, 2016

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KIJIJI RUGAZI MINZIRO KUKAGUA MADHARA YA TETEMEKO LA ARDHI

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (aliyevaa miwani) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigazi - akimweleza zaidi ya nyumba 200 zilizoanguka baada ya kutokea tetemeko la ardhi. Pichani ni nyumba ya Mzee John Paulo iliyoanguka baada ya kutokea tetemeko la ardhi. Zaidi ya kaya 300 hazina makazi. Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji Kigazi akibainisha changamoto wanazopambana nazo Wanakijiji cha Kigazi baada tetemeko la ardhi kutokea katika kijiji cha Kigazi.