Monday, September 5, 2016

DABI YA MANCHESTER JUMAMOSI HII - MANCHESTER UNITED vs MANCHESTER CITY: REFA NI MARK CLATTENBURG!

REFA Mark Clattenburg ametangazwa kuwa ndie atasimamia pambano la Ligi Kuu England, EPL, ambalo ni Dabi ya Manchester kati ya Mahasimu Manchester United na Manchester City itakayochezwa Uwanjani Old Trafford Jumamosi hii inayokuja.

Mbali ya kuwa hii ni Dabi, pia hii itakuwa ni Mechi ya kwanza kuwakutanisha Mahasimu wa tangu La Liga huko Spain ambao ni Mameneja wapya wa Klabu hizi za Jiji la Manchester wakati Pep Guardiola akiipeleka Man City Old Trafford kuivaa Timu inayoongozwa na Jose Mourinho, Man United.

Timu hizi zote zimeanza kwa kishindi kwenye EPL Msimu huu mpya kwa wao, pamoja na Chelsea, kuwa Timu pekee zilizoshindwa Mechi zao zote 3 za kwanza.
Refa Clattenburg hivi sasa nyota yake inang’ara kwani yeye ndio alikuwa Refa wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI Mwezi Mei wakati Real Madrid ikiibwaga Atletico Madrid na pia kusimamia Fainali ya EURO 2016 Mwezi Julai wakati Portugal ikiwafunga Wenyeji France na kutwaa Ubingwa wa Ulays.

Kwenye Dabi hii ya Manchester, Clattenburg atasaidiwa na Jake Collins na Steve Bennett wakati Refa wa Akiba ni Mike Dean.