Sunday, September 18, 2016

DTB KUSAINI MKATABA NA TFF

Benki inayokuja juu katika soko la fedha nchini Tanzania ya DTB (Diamond Trust Bank), kesho Jumatatu saa 4.30 asubuhi inatarajiwa kusaini mkataba wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuongeza udhamini katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hafla ya kusaini mkataba huo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, iliyoko kwenye makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Ohio jijini Dar es Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wanakaribishwa kwenye hafla hiyo itakayofanyika hotelini hapo.
IMETOLEWA NA TFF