Wednesday, September 21, 2016

EFL CUP: LEO NI NORTHAMPTON V MAN UNITED, NANI KUIBUKA KIDEDEA?

LEO Manchester United wapo ugenini huko Sixfields Stadium Jijini Northampton kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya EFL CUP, Kombe la Ligi, dhidi ya Timu ya Daraja la Ligi 1 Northampton Town.
Hii ni nafasi murua kwa Man United kufuta wimbi la kufungwa Mechi 3 mfululizo ndani ya Wiki moja.
Lakini Meneja wao, Jose Mourinho, amekataa kujiamini dhidi ya Timu ambayo iko Madaraja Mawili chini yao na ambayo sasa inashika Nafasi ya 11 kwenye Ligi 1 baada ya Majuzi kuchapwa 3-1 na Chesterfield na kumaliza wimbi lao la kutofungwa Mechi 31 lililoanza tangu Desemba 2015.

Kwenye Raundi ya Pili ya EFL CUP, Northampton Town iliibwaga Timu ya EPL, Ligi Kuu England, West Bromwich Albion kwa Penati.


EFL CUP
Raundi ya 3
Ratiba:
Jumatano Septemba 21 

Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku Saa za Bongo isipokuwa inapotajwa
Fulham v Bristol City
Northampton v Man United
QPR v Sunderland
Southampton v Crystal Palace
Swansea v Man City
West Ham v Accrington
2200 Stoke v Hull
2200 Tottenham v Gillingham