Friday, September 23, 2016

EPL: KESHO JUMAMOSI OLD TRAFFORD MAN UNITED v LEICESTER, TATHMINI NA UNDANI WA MECHI HIYO!

Jumamosi Mchana, Mechi ya kwanza kabisa ya EPL, Ligi Kuu England, ni Uwanjani Old Trafford wakati Wenyeji Manchester United wakicheza na Mabingwa wa England Leicester City.
Msimu uliopita, ambao Leicester walitwaa Ubingwa, Timu hizi zilitoka Sare Mechi zao zote 2 za Ligi.
Lakini tayari Msimu huu, Timu hizi zimeshavaana huko Wembley Stadium Jijini London katika Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Jamii ambayo kidesturi hugombewa na Bingwa wa England, ambae ni Leicester, na Bingwa wa FA CUP, ambae ni Man united.
Katika Mechi hiyo, Man United waliipiga Leicester 2-1 na kubeba Ngao ya Jamii.

JE WAJUA?
-Man United hawajafungwa katika Mechi 7 zilizopita dhidi ya Leicester Uwanjani Old Trafford wakishinda 5 na Sare 2 na mara ya mwisho Leicester kushinda hapo ilikuwa Januari 1998.
Man United watatinga kwenye Mechi hii wakiwakosa Majeruhi Anthony Martial na Phil Jones huku Henrikh Mkhitaryan akiwa kwenye hatihati wakati Leicester wanaweza kumkosa Kipa wao Kasper Schmeichel ambae ni Majeruhi na Marcin Wasilewski aliefungiwa Mechi 1.

NINI MAMENEJA WAMESEMA:
-Jose Mourinho [Man United]: ‘Kama Mashabiki walihuzunishwa Wiki iliyopita naelewa lakini nina haki Jumamosi watakuwa nyuma yetu!’

-Claudio Ranieri [Leicester]: ‘Sie hatuogopi Old Trafford! Zaidi ya kufungwa nini kitatokea? Nafurahia kucheza mbele ya Mashabiki 70,000! Sitaki twende huko kucheza mbele ya mimi na wewe tu, haitakuwa shoo kubwa!’
Kimsimamo kwenye EPL, Vinara ni Man City wenye Pointi 15 baada ya kushinda Mechi zao zote 5 na Man United wapo Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 9 na Leicester ni wa 11 wakiwa na Pointi 7.