Thursday, September 29, 2016

EUROPA EAGUE: MANCHESTER UNITED 1 v 0 ZORYA, ZLATAN IBRAHIMOVIV AIBEBA MAN OLD TRAFFORD LEO!


MAN UNITED wameifunga Zorya Luhansk ya Ukraine 1-0 katika Mechi yao ya pili ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.
Ushindi huu umeiweka Man United kwenye Reli baada ya kupoteza Mechi yao ya kwanza ya Kundi A huko Rotterdam walipofungwa na Feyenoord 1-0.
Bao la ushindi la Man United lilifungwa Dakika ya 69 kwa Kichwa na Zlatan Ibrahimovic kufuatia Krosi ya Fulbeki Fosu-Mensah kuunganishwa fyongo na Wayne Rooney na Mpira kudunda juu na Ibrahimovi kuumalizia.
Bao hilo lilikuja Dakika 2 tu baada ya Rooney kuingizwa Uwanjani kumbadili Jesse Lingard.
Kwenye Mechi nyingine ya Kundi A iliyochezwa huko Uturuki, Fenerbahce iliitungua Feyenoord 1-0.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Oktoba 20 na Fenerbahce Uwanjani Old Trafford.

Dakika ya 69 Zlatan Ibrahimovic aliipatia bao la ushindi la pekee kwenye mchezo huo ambao Timu ya Zorya iliucheza karibu wote kwa kulinda.http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0929/r133340_1296x729_16-9.jpg&w=904&h=509&scale=crop&site=espnfcPaul Pogba and Zlatan IbrahimovicPogba na Zlatan waanza