Thursday, September 15, 2016

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: ARGENTINA, BELGIUM BADO JUU, BRAZIL YAPANDA NI YA 4, TANZANIA YAPOROMOKA 8, IPO NAFASI YA 132!

Brazil sasa wamepanda hadi Nafasi ya 4 kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani ambayo Nambari Wani bado ni Argentina wakifuatiwa na Belgium huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 8 na kushika Nafasi ya 132.
Brazil wanashikana na Colombia katika Nafasi ya 4 baada ya kupanda Nafasi 5.
Mabingwa wa Dunia Germany wamepanda Nafasi 1 na sasa wapo Nafasi ya 3 wakati Chile, France na Portugal zikishuka Nafasi 1.

Uruguay wamepanda Nafasi 3 na kushika Nafasi ya 9 wakati Wales ikitumbukia 10 Bora baada ya Spain kuporomoka Nafasi 3 hadi ya kukaa Nafasi ya 11
England wamepanda Nafasi 1 na wapo wa 12 na Italy wameshuka 3 wakishika Nafasi ya 13.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa ni Ivory Coast ambao wako Nafasi ya 34 wakifuatia Algeria ambao wako wa 35.
Tanzania, ambayo ilishika Nafasi ya 124, sasa imeporomoka hadi Nafasi ya 132.
Listi ya FIFA ya Ubora Duniani inayofuatia itatolewa Oktoba 20.

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI – 10 BORA:
1. Argentina (Pointi 1646)
2. Belgium (1369)
3. Germany (1347)
4.- Colombia (1323)
4.-Brazil (1323)
6. Chile (1284)
7. Portugal (1228)
8. France (1188)
9. Uruguay (1173)
10. Wales (1161)