Friday, September 2, 2016

GUARDIOLA ‘AMKATA’ YAYA TOURE KIKOSI MAN CITY CHA UEFA CHAMPIONS

MANCHESTER CITY imemwacha Yaya Toure kwenye Listi ya Wachezaji wao watakaocheza UEFA CHAMPIONS LIGI, UZL, Msimu huu licha ya kusajili UEFA Wachezaji 21 ambao ni pungufu ya wale wanaoruhusiwa.
Msimu huu, chini ya Meneja mpya Pep Guardiola, Toure amecheza Mechi moja tu na ni ile ya Marudiano dhidi ya Steau Bucharest ambayo ilikuwa Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UCL.

City waliibwaga Steau Bucharest kwa kuichapa 5-0 katika Mechi ya kwanza na 1-0 kwenye Mechi ya pili na kutinga Makundi ya UCL ambapo wako Kundi moja pamoja na Borussia Monchengladbach, Celtic na Barcelona.
City wataanza kwao Etihad kwa kucheza na Borussia Monchengladbach hapo Septemba 13.
Tangu atue Guardiola, City imewaondoa kwa Mkopo Joe Hart, Wilfried Bony, Samir Nasri, Eliaquim Mangala na Jason Denayer na ilidhaniwa nae Toure atang’oka hasa baada ya Guardiola kumuuza Mchezaji huyo wa Ivory Coast walipokuwa wote huko Barcelona na kuhamia City Mwaka 2010.

Toure, mwenye Miaka 33, ametwaa Ubingwa wa England mara 2, FA CUP na Kombe la Ligi mara 2 akiwa na City.
MAN CITY – Kikoso kamili cha UCL:
Makipa:

Claudio Bravo, Willy Caballero
Mabeki:
Bacary Sagna, Vincent Kompany, Pablo Zabaleta, Aleksandar Kolarov, Gael Clichy, John Stones, Nicolas Otamendi

Viungo:
Fernando, Raheem Sterling, Ilkay Gundogan, Jesus Navas, Kevin De Bruyne, Fabian Delph, Leroy Sane, David Silva, Fernandinho

Mafowadi:
Nolito, Sergio Aguero, Kelechi Iheanacho