Monday, September 26, 2016

GUARDIOLA APATA PIGO, STAA WAKE KEVIN DE BRUYNE NJE MWEZI!

MANCHESTER CITY imepata pigo kubwa baada ya Nyota wao mkubwa hivi sasa Kevin De Bruyne kuthibitishwa atakuwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mmoja.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Belgium aliumia Musuli za Pajani (Hamstring) wakati City inaifunga Swansea City.3-1 huko Liberty Stadium hapo Jumamosi kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Msimu huu, chini ya Meneja wao mpya Pep Guardiola, De Bruyne amekuwa ndio nguzo yao kubwa iliyowapa ushindi katika Mechi zao zote 10 walizocheza hadi sasa.
Kukosekana kw Nyota huyo ni pigo kwa City kwenye kipindi hiki ambacho wana Mechi muhimu mno kuanzia ile ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI ya Kundi lao ya Jumatano Ugenini na Celtic.
Pia ataikosa mitanange ya EPL dhidi ya Tottenham na Everton.
Pia Staa huyo, ambae City walimnunua kwa Dau la Rekodi kwa Klabu yao la Pauni Milioni 55, yupo kwenye hatihati kuikosa Mechi ya Mwezi ujao ya UCL huko Nou Camp dhidi ya Barcelona ambayo ni Klabu ya zamani ya Guardiola.
De Bruyne huenda pia akaikosa Dabi ya Manchester Uwanjani Old Trafford hapo Oktoba 25 dhidi ya Manchester United ikiwa ni Raundi ya 4 ya EFL CUP.
Msimu huu, De Bruyne, mwenye Miaka 25, amefunga Bao 2 na kutengeneza kadhaa akiwa ndani ya uti wa City katika mafanikio yao hadi sasa.
Hivi karibuni Guardiola alitamba De Bruyne yuko juu pamoja na Lionel Messi katika ngazi ya Ubora Duniani.