Friday, September 16, 2016

KILIMANJARO QUEENS KUMENYANA NA UGANDA NUSU FAINALI CHALLENGE

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara ya wanawake, Kilimanjaro Queens imemaliza kwa sare ya bila kufungana katika mechi za Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mjin Jinja leo.
Kwa matokeo hayo, Kilimanjaro Queens itamenyana na wenyeji Uganda katika Nusu Fainali Jumapili, wakati Nusu Fainali nyingine itazikutanisha Kenya vs Ethiopia.
Fainali ya CECAFA Challenge ya kwanza ya wanawake inatarajiwa kufanyika Septemba 20, ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.