Tuesday, September 20, 2016

KILIMANJARO QUEENS MABINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI, YAIBWAGA KENYA FAINALI!

BAO 2 safi za Winga Mwahamisi Omari zimewapa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Kenya kwenye Fainali ya Mashindano ya CECAFA ya kugombea Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Kinamama iliyochezwa huko FUFA Technical Center, Njeru, Mjini Thika Nchini Uganda.
Bao hizo mbili za Mwanahamisi zilifungwa Dakika za 26 na 45 na kuwafanya Kilimanjaro Queens waende Mapumziko wakiwa mbele 2-0.
Bao la Kenya, maarufu kama Harambee Starlets, lilifungwa Dakika ya 50 na Christine Nafula.
Kilimanjaro Queens ilitinga Fainali kwa kuwatoa Wenyeji Uganda 4-1 na Harambee Starlets kuibwaga Ethiopia 3-2.

Kilimanjaro Queens, chini ya Kocha Sebastian Nkoma, walitoka Kundi B pamoja na Rwanda na Ethiopia, na wao kufuzu kama Washindi wa Kundi baada ya Kura ya Shilingi kufuatia kulingana kila kitu na Ethiopia.