Wednesday, September 21, 2016

KILIMANJARO QUEENS WATUA BUKOBA LEO NA MWALI WAO KUTOKEA NCHINI UGANDA.


Mabingwa wapya wa Kombe la Chalenji la CECAFA, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens, mara baada ya kutua hapa Mjini Bukoba leo Asubuhi wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera , Meja Jenerali mstaafu Salum Kujuuna kuwapongeza kwa Ushindi huo mkubwa walioupata kwa kuifunga Timu ya Kenye bao 2-1.

Timu hii inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho Septemba 22, 2016 saa 7.00 mchana kwa ndege ya FastJet ikitokea Mwanza.
Mara baada ya kutua, itakwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya Coartyard iliyoko Sea View, Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambako watakuwako viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wale wa Serikali akiwamo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi.Ni baada ya kuwaunga Timu ya Kenya bao 2-1.

BAO 2 safi za Winga Mwahamisi Omari zimewapa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Kenya kwenye Fainali ya Mashindano ya CECAFA ya kugombea Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Kinamama iliyochezwa huko FUFA Technical Center, Njeru, Mjini Thika Nchini Uganda.
Bao hizo mbili za Mwanahamisi zilifungwa Dakika za 26 na 45 na kuwafanya Kilimanjaro Queens waende Mapumziko wakiwa mbele 2-0.
Bao la Kenya, maarufu kama Harambee Starlets, lilifungwa Dakika ya 50 na Christine Nafula.
Kilimanjaro Queens ilitinga Fainali kwa kuwatoa Wenyeji Uganda 4-1 na Harambee Starlets kuibwaga Ethiopia 3-2.

Kilimanjaro Queens, chini ya Kocha Sebastian Nkoma, walitoka Kundi B pamoja na Rwanda na Ethiopia, na wao kufuzu kama Washindi wa Kundi baada ya Kura ya Shilingi kufuatia kulingana kila kitu na Ethiopia.