Sunday, September 25, 2016

KISAGO TOKA KWA ARSENAL: CONTE ALIA CHELSEA KURUHUSU MAGOLI! ASEMA WATA DIFENSI YAKE HAIKUWEKA MKAZO!

Antonio Conte, Meneja wa Chelsea, amelalama juu ya Uchezaji wa Timu yake kufuatia Jana kuchapwa 3-0 na Arsenal Timu ambayo kwenye EPL, Ligi Kuu England, ilikuwa 'Mteja wake' wa kawaida.
Jana huko Emirates Bao za Kipindi cha Kwanza za Alexis Sanchez, Theo Walcott na Mesut Ozil ziliwapa Arsenal ushindi huo ambao ni wa kwanza kwa Arsenal dhidi ya Chelsea tangu Oktoba 2011.
Conte amelalamika: "Lazima tufanye kazi kwa bidii kwani sisi ni Timu nzuri kwenye karatasi tu! Kuanzia Dakika ya Kwanza uchezaji wetu haukuwa na mkazo mzuri!"
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Chelsea kwenye EPL ambacho kimewaacha Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 8 nyuma ya Vinara Man City.
Conte alinyooshea kidole udhaifu wa Difensi yao na kusema inahitaji kujirekebisha haraka.
Jana walimkosa Nahodha wao John Terry ambae ni Sentahafu ambae sasa ni Majeruhi na Jana pozisheni hiyo kushikwa na Gary Cahill, aliefungisha Bao 1, na David Luiz ambae aliyumba mno.
Conte ameeleza: "Hatuna uwiano mzuri na sasa ni wakati wa kutafakari vizuri. Ni ajabu kuruhusu Bao 3! Lazima tutafute jawabu!"
Kuhusu wao kuwemo mbio za Ubingwa, Conte alipanchi swali hilo na kusema ni juu yao kurudia upya mtiririko wa ushindi.
Ameeleza: "Kitu muhimu kabisa ni kufanya kazi na kutofikiria hali hii!"