Tuesday, September 6, 2016

KOMBE LA DUNIA 2018: MABINGWA ULAYA PORTUGAL LEO KUANZA SAFARI YA URUSI, FRANCE, HOLLAND, BELGIUM NAZO DIMBANI!

MABINGWA wa Ulaya Portugal Usiku huu wa Leo wapo Ugenini kucheza Mechi yao ya kwanza ya Kundi B ya Nchi za Ulaya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia kwa kucheza na Switzerland.
Portugal watatinga kwenye Mechi hii bila ya Mchezaji Bora wa Ulaya Cristiano Ronaldo ambae sasa anajiuguza Goti aliloumia Mwezi Julai wakati Portugal ikiifunga France katika Fainali ya EURO 2016.
Mechi nyingine za Kundi B ni kati ya Faroe Islands na Hungary na ile ya Andorra v Latvia.
Mtanange mkali uko katika Kundi A wakati Sweden wakiikaribisha Netherlands wakati Mechi nyingine za Kundi hili ni Bulgaria na Luxembourg na nyingine ni Belarus wakiikaribisha France.
Pia zipo mechi 3 za Kundi H kati ya Bosnia and Herzegovina na Estonia, Cyprus wakiivaa Belgium na Gibraltar kucheza na Greece.
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Septemba 4

Kundi C: San Marino 0 Azerbaijan 1
Kundi E: Denmark 1 Armenia 0, Kazakhstan 2 Poland 2
Kundi F: Slovakia 0 England 1, Lithuania 2 Slovenia 2
Kundi C: Czech Republic 0 Northern Ireland 0, Norway 0 Germany 3
Kundi E: Romania 1 Montenegro 1
Kundi F: Malta 1 Scotland 5

Jumatatu Septemba 5
Kundi D:
Georgia 1 Austria 2
Kundi D: Wales 4 Moldova 0, Serbia 2 Republic of Ireland 2
Kundi G: Spain 8 Liechtenstein 0, Albania 1 FYR Macedonia 1, Israel 1 Italy 3
Kundi I: Finland 1 Kosovo 1, Croatia 1 Turkey 1, Ukraine 1 Iceland 1

Jumanne Septemba 6
21:45 (Saa za hapa tz)
Kundi A: Bulgaria v Luxembourg, Sweden v Netherlands, Belarus v France
Kundi B: Switzerland v Portugal, Faroe Islands v Hungary, Andorra v Latvia
Kundi H: Bosnia and Herzegovina v Estonia, Cyprus v Belgium, Gibraltar v Greece