Sunday, September 18, 2016

KUZIONA SERENGETI BOYS NA CONGO BRAZZAVILLE NI BUREEE..... LEO UWANJA WA TAIFA

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Serengeti Boys katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 unapigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa dhidi ya Timu ya vijana ya Congo-Brazzaville. Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mhe. Nape amesema milango ipo wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri katika mechi hii ambayo ni muhimu sana kushinda