Friday, September 16, 2016

LIGI KUU ENGLAND: LEO NI IJUMAA NI CHELSEA vs LIVERPOOL

Ligi Kuu England, inaanza Mechi zake za Wikiendi hii Leo Usiku huko Jijini London Uwanjani Stamford Bridge pale Wenyeji Chelsea watakapocheza na Liverpool.
Chelsea, chini ya Meneja Mpya kutoka Italy Antonio Conte, hawajafungwa Msimu huu na wapo Nafasi ya Pili na wanapambana na Liverpool ya Mjerumani Jurgen Klopp iliyofungwa Mechi 1.

Kileleni wapo Man City walioshinda Mechi zao zote 4 na wana Pointi 12, wanafuata Chelsea wakiwa Pointi 2 nyuma wakifungana na Everton na kisha ni Man United ambao wako Pointi 1 nyuma yao huku Liverpool wakiwa Nafasi ya 6.
JE WAJUA?
-Chelsea wamefungwa Mechi 1 tu katika Mechi 8 zilizopita za Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool [Wameshinda 3 Sare 4 Kipigo 1].

-Kipigo pekee ni Oktoba 2015, Meneja Mpya Jurgen Klopp alipopata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Chelsea Uwanjani Stamford Bridge.
Kwenye Mechi hii, Chelsea imempoteza Kepteni wao John Terry, mwenye Miaka 35, alieumia Jumapili iliyopita wakati Chelsea ikitoka Sare 2-2 na Swansea huko Liberty Stadium katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Lakini hii ni nafasi murua kwa Sentahafu wao mpya, David Luiz, ambae amesainiwa tena na Chelsea safari hii akitokea Paris St-Germain ya France.
Luiz, Raia wa Brazil, aliuzwa na Chelsea huko PSG Miaka Miwili iliyopita kwa Dau la Pauni Milioni 50 ambalo ni rekodi kwa Beki kununuliwa Bei ghali kiasi hicho.

Chelsea walimnunua Luiz kwa mara ya kwanza Januari 2011 kutoka Benfica kwa Pauni Milioni 21 na akadumu Miaka Mitatu na kucheza Mechi 143 akifunga Bao 12.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
CHELSEA [4-2-3-1]:

-Courtois
-Ivanovic, Cahill, Luiz, Azpilicueta
-Matic, Kante
-Willian, Hazard, Oscar
-Costa

LIVERPOOL [4-3-3]:
-Mignolet
-Clyne, Lovren, Matip, Milner
-Lallana, Henderson, Wijnaldum
-Mane, Sturridge, Coutinho
REFA: Martin Atkinson

LIGI KUU ENGLANDRATIBA
Ijumaa Septemba 16

2200 Chelsea v Liverpool
Jumamosi Septemba 17
1700 Hull City v Arsenal
1700 Leicester City v Burnley
1700 Man City v Bournemouth
1700 West Bromwich Albion v West Ham
1930 Everton v Middlesbrough

Jumapili Septemba 18
1400 Watford v Man United
1615 Crystal Palace v Stoke
1615 Southampton v Swansea 

1830 Tottenham v Sunderland