Thursday, September 22, 2016

LIONEL MESSI NJE WIKI 3!

MABINGWA wa La Liga Jana huko kwao Nou Camp walitoka Sare 1-1 na Atletico Madrid na pia kumpoteza Lionel.Messi ambae alitoka baada ya kuumia.
Taarifa toka Barca zimedokeza kuwa Messi atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3 akiuguza Nyonga yake.
Kwenye Mechi hiyo, Barca walitangulia kufunga kwa Bao la Kipindi cha Kwanza la Ivan Rakitic aliefunga kwa Kichwa akiunganisha krosi ya Iniesta.
Kipinĸi cha Pili Majeruhi yakawafanya Barca wawapoteze Sergio Busquets na kisha Messi na kutoa mwanya kwa Correa kusawazisha kutokana na kosa la Javier Mascherano.

Matokeo hayo yamewaweka Barca Nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Vinara Real Madrid kwa Pointi 3 huku Nafasi ya Pili ikishikwa na Sevilla walio Pointi 2 nyuma ya Real na Atletico wapo Nafasi ya 4 Pointi 1 nyuma ya Barcam
Mapema Jana Real walibanwa na kutoka 1-1 na Villareal.
Villareal walitangulia kufunga kwa Penati ya Bruno Soriano ya Kipindi cha Kwanza ya baada ya Sergio Ramos kuunawa Mpira lakini mwanzoni Kipindi cha Pili Ramos akafuta makosa yake kwa kusawazisha.