Saturday, September 24, 2016

FULL TIME: ARSENAL 3 v 0 CHELSEA


ARSENAL Leo wameondoa gundu la kutoifunga Chelsea kwenye EPL, Ligi Kuu England, baada ya kuwachapa 3-0 Uwanjani Emirates.
Mara ya mwisho kwa Arsenal kuwafunga Chelsea kwenye Ligi ni 5-3 huko Stamford Bridge Mwaka 2011.
Arsenal walianza Mechi hii kwa moto na
Dakika ya 11 Alexis Sanchez alifunga Bao safi kufuatia makosa ya Sentahafu Gary Cahill na Dakika 3 baadae ushirikiano mzuri wa Iwobi na Bellerin ulimfikia Theo Walcott aliepachika Bao la Pili.
Bao la 3 kwa Arsenal lilifungwa Dakika ya 40 na Mesut Ozil alieanzisha kaunta ataki na kumpa Sanchez aliemrudishia tena Sanchez na kufunga Bao safi.
Hadi Mapumziko Arsenal 3 Chelsea 0.

Bao hizo 3 zilisimama hadi Mpira kwisha na kuwasimika Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Tottenham na 5 nyuma ya Vinara Man City.
Kwa Chelsea hiki ni kipigo cha Pili mfululizo kwenye EPL baada ya pia kuchapwa na Liverpool 2-1 na sasa wameshuka hadi Nafasi ya 8.
JE WAJUA?
-Arsenal walikuwa hawajawafunga Chelsea kwa Miaka 5 kwenye Ligi na kwa Misimu Mitatu iliyopita walishindwa hata kupata Bao 1.
-Msimu uliopita, ambao Chelsea walikuwa nyang’anyang’a, Arsenal walipigwa Mechi zote 2 za Ligi.