Friday, September 16, 2016

FULL TIME..CHELSEA 1 vs 2 LIVERPOOL, DEJAN LOVREN NA HENDERSON NA WENZAKE WAWACHEZEA MPIRA MKUBWA BLUES KWAO DARAJANI!A


BAO 2 za Kipindi cha Kwanza kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, huko Jijini London Uwanjani Stamford Bridge zimewafanya Wenyeji Chelsea wafungwe Mechi yao ya kwanza ya Ligi walipolala 2-1 toka kwa Liverpool.
Msimu uliopita, Mwezi Oktoba chini ya Meneja Jurgen Klopp, Liverpool waliifunga Chelsea hapo hapo Stamford Bridge na safari hii Bao za Dejan Lovren na Jordan Hendrson ziliwafanya waongoze 2-0 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Chelsea, wakicheza bila ya Kepteni wao Majeruhi John Terry na nafasi yake kuchukuliwa ns ‘mpya’ David Luiz, walifunga Bao lao kupitia Diego Costa na kulala 2-1.

Msimu huu, Jijini London, Chelsea waliipiga Arsenal 4-3 huko Emirates na kutoka Sare na Tottenham.
Wiki iliyopita, huko Anfield, Liverpool waliwatwanga Mabingwa Watetezi Leicester City 4-1.
Dejan Lovren dakika ya (17')
Jordan Henderson dakika ya (36') mpaka dakika ya mapumziko inafika Liverpool walikuwa wanaongoza 2-0 dhidi ya Chelsa ambao wako kwao Darajani.
Wakipongezana kwa baoLovren dakika ya 17 aliifungia bao Liverpool