Sunday, September 18, 2016

FULL TIME: WATFORD 3 vs 1 MANCHESTER UNITED, NI SHEREHE KWA WATFORD LEO...WAWEKA REKODI KUIFUNGA UNITED!

Watford vs Manchester United, English Premier League LIVE score 2016:
WAKICHEZA Ugenini huko Vicarage Road Manchester United Leo wamefungwa Bao 3-1 na Watford kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Hii ni mara ya kwanza kwa Watford kuifunga Man United katika Miaka 30.
Bao za Watford zilufungwa Dakika za 34, 83 na Penati ya Dakika ya 94 kupitia Etiene Capoye, Juan Zaniga na Troy Deeney.
Bao la Man United lilufungwa na Marcus Rashford katika Dakika ya 62.
Kwenye EPL hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Man United baada ya Wikiendi iliyopita kufungwa pia na Man City lakini pia Juzi kati Wiki walichapwa 1-0 huko Rotterdam na Feyenoord kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao la UEFA EUROPA LIGI.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumatano Ugenini na Northampton ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 3 ya EFL CUP ambalo ni Kombe la Ligi.

Watford ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 34 kupitia kwa Etienne Capoue (34') Na kipindi cha pili dakika ya 62
Marcus Rashford aliiswazishia bao Man United na kufanya bao kuwa 1-1.Bao la tatu kwa Watford lilikuwa la mkwaju wa penati dakika za nyongeza za kumalizia  dakika 90 na mtanange kumalizika kwa  3-1.