Sunday, September 11, 2016

FULL TIME....SWANSEA CITY 2 v 2 CHELSEA

STRAIKA wa Chelsea Diego Costa aliisawazishia Chelsea katika Dakika ya 81 na kupata Sare ya 2-2 walipocheza Ugenini na Swansea City huko Liberty Stadium katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Chelsea walitangulia kwa Bao 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Diego Costa.
Lakini, katika Dakika 2 za Kipindi cha Pili, Swansea waliigeuza Mechi na kupiga Bao 2 na kuongoza 2-1.
Bao la kwanza Swansea lilifungwa na Gylfi Sigurdsson kwa Penati iliyotolewa baada yeye mwenyewe kuangushwa na Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois na Dakika 2 baadae Leroy Fer kuweka Bao la Pili baada ya makosa makubwa ya Gary Cahill.