Thursday, September 29, 2016

Maafa Kagera yapadisha Maafisa Wa Benki ya CRDB, RAS na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba


Maafisa watatu wa serikali akiwa Afisa Tawala mkoa wa Kagera, (RAS), Amantius Msole, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, na meneja wa benki ya CRDB tawi la Bukoba wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Bukoba leo Septemba 29, 2016wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama kwa kufungua akaunti ya bandia inayofanana na ile inayotumika kukusanya fedha za waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo Septemba 10, 2016.

RAS Amantius Msole (katikati), na watuhumiwa wenzake wakisindikizwa na maaskari kanzu kuelekea mahakamani leo

Watuhumiwa wakiwa kwenye chumba cha mahakama wakisubiri shauri lao

RAS Amantius Msole, (wakwanza kushoto), akijadiliana jambo na wakili wake