Friday, September 2, 2016

MAN CITY WAPATA PIGO KUBWA: AGUERO ‘JELA’ MECHI 3, KUIKOSA DABI NA MAN UNITED OLD TRAFFORD SEP 10!

STRAIKA wa Manchester City Sergio Aguero ataikosa Dabi ya Manchester Jumamosi inayokuja ya Septemba 10 dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Manchester United Uwanjani Old Trafford baada ya kufungiwa Mechi 3.
Hii Leo, Jopo Huru la Ligi Kuu England, EPL, lilimkuta ana hatia ya Uchezaji wa Fujo kwa kumpiga Kipepsi Beki wa Beki wa West Ham Winston Reid na kutoa Adhabu hiyo licha ya Klabu yake kukataa Mashitaka hayo.
Tukio hilo lilitokea Dakika ya 76 ya Mechi ya Jumapili iliyopita huko Etihad na Refa Andre Marriner hakuliona lakini lilimfanya Reid atoke nje akishika shingo yake na kutibiwa na kutorudi tena Uwanjani baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Mchezaji mwingine.
FA, Chama cha Soka England, kilipitia Mkanda wa Video wa Tukio hilo na kuamua kulipeleka kwa Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani ambao kwa pamoja waliridhika kuwa Kosa hilo lilistahili Kadi Nyekundu kama Refa angeliliona na hivyo FA kuwajibika kumfungulia Mashitaka Aguero.

Mechi nyingine ambazo Aguero, mwenye Miaka 28, ambazo atazikosa ni zile za EPL na Bournemouth Uwanjani Etihad na ile ya Ugenini ya Raundi ya 3 ya EFL CUP dhidi ya Swansea City.
Msimu huu kwenye EPL, Aguero ameifungia City Bao 3 katika Mechi zao 3 na kuwaweka kileleni wakiwa Pointi sawa na Man United na Chelsea ambao wote wameshinda Mechi zao zote 3 hadi sasa.

Pia Aguero alipiga Hetitriki wakati City inaicharanga Steaua Bucharest 5-0 huko Romania kwenye Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI.