Friday, September 2, 2016

MAN UNITED: BASTIAN SCHWEINSTEIGER KIKOSINI TIMU YA KUCHEZA LIGI KUU ENGLAND 2016/17!

KIUNGO na aliekuwa Nahodha wa Germany Bastian Schweinsteiger ni miongoni mwa Wachezaji 25 wa Manchester United ambao wamesajiliwa rasmi kwa ajili ya Ligi Kuu England, EPL, kwa Msimu huu wa 2016/17.
Schweinsteiger, mwenye Miaka 32 na ambae aliiongoza Germnay Mwaka 2014 kutwaa Kombe la Dunia huko Brazil, alitajwa na Meneja Jose Mourinho kuwa yupo kwenye hatihati kutoichezea tena Timu hiyo.
Mapema Wiki hii, Schweinsteiger alistaafu rasmi kuichezea Germany baada ya kucheza Mechi 121 na kufunga Bao 24.
Kwa mujibu wa Kanuni za EPL, Klabu zote 20 za EPL zilipaswa kupeleka Majina 25 ya Wachezaji wao.

Schweinsteiger, ambae alitua Man United Julai 2015, amekuwa hafanyi Mazoezi na Kikosi cha Kwanza tangu Mourinho aanze kazi yake.
Lakini mwenyewe ameshasema kuwa yeye yupo tayari kuichezea Man United wakati wowote ule.

MAN UNITED – Kikosi kamili cha EPL: Eric Bailly, Daley Blind, Michael Carrick, Matteo Darmian, David De Gea, Memphis Depay, Sadik El-Fitouri, Marouane Fellaini, Ander Herrera, Zlatan Ibrahimovic, Sam Johnstone, Phil Jones, Jesse Lingard, Juan Mata, Henrikh Mkhitaryan, Paul Pogba, Marcos Rojo, Sergio Romero, Wayne Rooney, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Chris Smalling, Antonio Valencia, Ashley Young
EPL kwa sasa ipo Mapumzikoni kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki 2 na Mechi inayofuata ni Manchester Dabi kati ya Man United na Man City ndani ya Old Trafford.