Monday, September 12, 2016

MAN UNITED YAWEKA REKODI YA KUWA TIMU YA KWANZA KUINGIZA MKWANJA MREFU UINGEREZA.


KLABU ya Manchester United imeweka rekodi ya mapato ya kiasi cha paundi milioni 515.3 katika mwaka wa fedha wa 2016, ikiwa ni klabu ya kwanza kwa Uingereza kufanya hivyo. Kwa mwaka huu wakati waliposhinda taji la Kombe la FA, klabu hiyo ya Old Trafford pia imesaini mikataba 14 ya udhamini na kushuhudia mapato ya mechi, biashara na TV yote yakikua. Sasa inatabiriwa kuwa mpaka kufikia mwaka 2017 mapato yatakuwa zaidi ya paundi milioni 540, hata kama hawapo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Chini ya meneja mpya Jose Mourinho, United kwasasa inashikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu.