Monday, September 12, 2016

MARIO BALOTELLI APIGA 2 MECHI YA KWANZA NICE, ASEMA LIVERPOOL ILIKUWA NI KOSA KUBWA KUJIUNGA NAYO!!

Mario Balotelli Jana aliifungia Timu yake ya Mkopo Nice ya France Bao 2 katika Mechi yake ya kwanza walipoilaza Marseille 3-2 kwenye Ligi 1 na kudai kujiunga na Liverpool lilikuwa kosa kubwa katika maisha yake.
Balotelli, ambae aliihama Liverpool Siku ya Mwisho ya Uhamisho Agosti 31, alifunga Bao la kwanza hiyo Jana kwa Penati katika Dakika ya 7 likiwa ni Bao lake la kwanza kwenye Ligi tangu tangu Septemba 22 Mwaka Jana.

Marseille walisawazisha Bao hilo na kufunga la Pili kupitia Florian Thauvin na Bafetimbi Gomis lakini zikibaki Dakika 12, Balotelli aliisawazishia Nice na Wylan Cyprien kuipigia Bao la 3 na ushindi katika Dakika ya 87.
Bao 2 kwa Nice katika Dakika 78 zimepiku Msimu wake mzima aliokuwa na Liverpool na kufunga Bao 1 tu dhidi ya Tottenham Hotspur.

Akihojiwa na Kituo cha TV cha France cha Canal Plus kuhusu nini kimeenda kombo katika maisha yake, Balotelli, mwenye Miaka 26, alisema: “Nilijiunga na Liverpool. Ni kosa kubwa katika maisha yangu. Mbali ya Mashabiki, ambao walikuwa wema kwangu, lazima niwe mkweli, na Wachezaji wenzangu, ambao tuliishi vizuri, sikuipenda Klabu ile!” “Nilikuwa na Makocha Wawili, Brendan Rodgers na J├╝rgen Klopp. Sikuona uzuri wao. Hatukupatana!”