Friday, September 16, 2016

MOURINHO HANA WASIWASI NA MAN UNITED KUFUNGWA MECHI YA PILI MFULULIZO!

Jose Mourinho amesema hana wasiwasi wowote kwa kufungwa Ugenini huko Rotterdam 1-0 na Feyenoord katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.
Hii ni Mechi ya Pili mfululizo kwa Man united baada ya Jumamosi iliyopita kufungwa 2-1 na Man City kwenye EPL, Ligi Kuu England.
Amesema: “Ni wazi sina furaha na mwanzo wetu. Kipindi cha Pili tulitawala. Goli lao ni Ofsaidi ya wazi!”
Alipoulizwa kuhusu kubadili Kikosi chake, Mourinho alijibu: “Tizama sitaki kumtaja Mtu. Baadhi ya Wachezaji ndio kwanza walikuwa wakianza kucheza mechi zao za kwanza za Msimu!”

Kuhusu Mechi yao ya Jumapili Ugenini na Watford ya EPL, Ligi Kuu England, Mourinho alieleza: “Ni wazi nimewaacha Wachezaji kama Valencia na Shaw Nyumbani ili wapumzike na tutarudi Timu yetu ya kawaida.”
Kwenye Mechi hiyo na Feyenoord, Meneja wa Man United Jose Mourinho aliamua kupangua Kikosi chake cha kawaida kwa kuwapumzisha Wachezaji 8 na kubakisha Watatu tu, Kipa De Gea, Sentahafu Eric Bailly na Pogba, kwa kuwatumia Wachezaji ambao wamekuwa hawana namba Msimu huu.


MAN UNITED – Mechi zao za Kundi A:

MD 1 – Alhamisi Sep 15 – Feyenoord 0 Man United 1
MD 2 – Alhamisi Sep 29 22:05 – Man United v Zorya Luhansk
MD 3 – Alhamisi Okt 20 22:05 – Man United v Fenerbahce SK
MD 4 – Alhamisi Okt 27 2000 – Fenerbahce SK v Man United
MD 5 – Alhamisi Nov 24 2305 – Man United v Feyenoord
MD 6 – Alhamisi Des 8 2100 – Zorya Luhansk v Man United