Sunday, September 4, 2016

MSANII LADY JAY DEE AKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA JIJI LA MWANZA.


Jana jumamosi Septemba 03,2016 kuamkia leo jumapili, Msanii nguli nchini, Lady Jay Dee (katikati) akiwa na bendi yake ya "Machozi Band" alikonga nyoyo za wapenzi wa burudani Jijini Mwanza, baada ya kuwadondoshea burudani murua kwenye show yake aliyoipa jina la "Naamka Tena Tour".

Mashabiki wa Lady Jay Dee, Binti Komando kama wengi wanavyomuita, walifurahia nyimbo mbalimbali, kuanzia zile za kitambo hadi nyimbo mpya.

Muziki ulipigwa #Live na watu walifurahia Show ambapo baada ya takribani masaa mawili ya burudani ya Jay Dee, bado wengine walisikika wakisema "Rudia Tenaaaa"
Timu ya Wananzengo wa 102.5 Lake Fm Mwanza, ilikuwepo kwenye show hiyo. Lake Fm Fm ilitoa mchango mkubwa wa kutangaza show hiyo

Imeandaliwa na BMG