Sunday, September 11, 2016

MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA ADOLPH KOLPING ENGLISH MEDIUM PRIMARY(AKEMPS) 2016

Mgeni Rasmi Bw. Karlo A. Sendwa ambaye ni Meneja CRDB Benki Tawi la Bukoba(katikati) kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Sr. Marcelina Masha(kushoto) ni Mh. Renatus Rwekaza ambaye ni Mwenyekiti wa Shule hiyo ijulikanayo zaidi kwa jina la AKEMPS wakati wa Mahafali hayo ya tano yaliyofanyika kwenye Shule hiyo siku ya jumamosi sept. 10, 2016.
Wahitimu
Mh. Renatus Rwekaza ambaye ni Mwenyekiti wa Shule ya AKEMPS Akitoa neno kwa Wahitimu na kwa Wazazi kiujumla wakati wa Mahafali hayo.
Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Adolph Kolping English Medium iliyopo iliyopo maeneo ya Ihungo Kilometa 8 kutoka Bukoba mjini wakisoma risala yao kwa Mgeni Rasmi Bwana Karlo A. Sendwa ambaye ni Meneja CRDB Benki Tawi la Bukoba wakati wa mahafali ya tano, Kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Mgeni Rasmi Bwana Karlo A. Sendwa ambaye ni Meneja CRDB Benki Tawi la Bukoba(kushoto) akiwa na Mkuu wa Shule hiyo Sr. Marcelina Masha wakiwa makini kuwasikiliza wahitimu hao kwa risala yao.
Mgeni Rasmi Bwana Karlo A. Sendwa ambaye ni Meneja CRDB Benki Tawi la Bukoba(kushoto) akiwa na Mkuu wa Shule hiyo Sr. Marcelina Mashawakiteta jambo wakati wa Mahafali hayo. Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba.Zoezi la Vyeti likiendelea
Malimu akiwaongoza Wanafunzi wa Shule ya Kolping wakati wa Misa wakiimba nyimba za kumsifu na Kumtukuza Bwana wakati wa Misa ikiendelea Shuleni hapo wakati wa Mahafali ya Darasa la saba.

Viongozi wa dini: Mapadre wakiendesha Misa wakati wa Mahafali hayo ya tano kwenye shule hiyo ya AKEMPS siku ya jumamosi Septemba 10, 2016

Mzazi wa mhitimu akifuatilia kwa karibu Mahafali hayo ambayo yalitanguliwa na Misa

Mahali hayo yalitanguliwa na Misa