Sunday, September 4, 2016

PGMOL YAKANUSHA MADAI YA REFA WA ZAMANI YA KULAZIMISHWA KUDANGANYA!

Professional Game Match Officials Limited (PGMOL), Kampuni inayosimamia Marefa huko Uingereza, imekanusha vikali madai ya Refa wa zamani Mark Halsey kwamba aliwahi kuambiwa aseme hakuona tukio kwenye Mechi ili Mchezaji aadhibiwe na Jopo Huru la FA, Chama cha Soka England.
Halsey, ambae alistaafu Urefa Mwaka 2013, aliibua tuhuma hizo kwenye mabishano Mtandaoni Twitter walipozungumzia kushitakiwa kwa Fowadi wa Man City Sergio Aguero ambae alifunguliwa Mashitaka na FA baada ya Refa Andre Marinner kukiri kutoona tukio la Aguero kumpiga Kipepsi Winston Reid kwenye Mechi ya Ligi Kuu England kati ya City na West Ham.
Kwa mujibu wa Kanuni huko England, ikiwa Refa atabainisha hakuona tukio kama hilo basi Mchezaji Mhusika hufunguliwa Mashitaka na
FA, na baada kupitia Mkanda wa Video wa Tukio hilo kama la Aguero na kuamua kulipeleka kwa Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani ambao kwa pamoja wakiridhika kuwa Kosa hilo lilistahili Kadi Nyekundu kama Refa angeliliona na hivyo FA kuwajibika kumfungulia Mashitaka.

Kwenye Twitter Halsey alisema: "Nimewahi kuwa kwenye hali kama hiyo na kuliona tukio na kuambiwa niseme sikuliona! Na sio FA wanaokutaka useme hivyo ni PGMOL!" Lakini taarifa kutoka PGMOL imekanusha madai hayo na kusema Marefa wanawasilisha Ripoti zao za Mechi moja kwa moja kwa FA na PGMOL haiwapi presha kuandika wanachotaka wao